Tukio la kuwaaga wanajeshi 14 wa Tanzania waliokuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo zime
fanyika jiji Dar es Salaam.
fanyika jiji Dar es Salaam.
Wanajeshi hao waliuawa baada ya kupiga na waasi kwa muda wa saa 13 kufuatia waasi hao kuishambulia kambi yao.
Sherehe hizo zimefanyika kwenye makao makuu ya jeshi la ulinzi na usalama Tanzania "gnome" upanga jijini Dar es Salaam
Mkuu wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa Jean Piare Lacroix, alihudhuria sherehe hizo. Familia za wanajeshi hao nazo zilikuwepo na zimeungana na wapendwa wao kuelekea mikoani.
Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.
Umoja wa Mataifa unasema waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Comments
Post a Comment